Paul Pogba kurejea Juventus!

Paul Pogba kurejea Juventus!


Imeripotiwa nyota wa Manchester United, Paul Pogba ameiyambia klabu yake kuwa anahitaji kurejea kwenye timu yake ya zamani ya Juventus kwenda kucheza pamoja na Cristiano Ronaldo.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Marca, Pogba amemueleza wakala wake kuwa anahitaji kurejea Juve kwenda kucheza na Ronaldo licha klabu ya Barcelona ikihusishwa kumuhitaji mchezaji huyo.

Mara baada ya kuonja mafanikio ya kutwaa kombe la dunia nchini Urusi, Paul Pogba anahitaji kuendeleza moto huo hadi kwenye levo ya klabu na hivyo akihitaji kuchana na Jose Mourinho ndani ya Manchester United na kurejea Juventus.

Miaka miwili iliyopita United ilitoa kiasi cha euro milioni 114 kukamilisha usajili wa Mfaransa huyo, Pogba akitokea Juve.

Kutua kwa Ronaldo Juventus kumeleta mabadiliko makubwa mno ndani ya klabu hiyo ya Italia licha tu ya kushawishika kwa Pogba lakini pia tiketi za mauzo kwa mashabiki zote zimekwisha ni kutokana uwepo wa nyota huyo.

Comments

Popular Posts